(Zanzibar, Julai 15, 2012). Zuku usiku wa kuamkia leo ilifanikiwa kuaanda warsha ya watengenezaji filamu kutoka baadhi za nchi mbali mbali, ambao wanahudhuria Tamasha la 15 ya Zanzibar International Film Festival ZIFF.
Kauli mbiu ya warsha hiyo ilikuwa “Kupandisha viwango vya ubora katika filamu za kiafrika”. Wadau hao walilenga kuangalia kwa undani majukumu mbalimbali kuanzia kwa wawekezaji, watangazaji, na wazalishaji kwa lengo la kutoa ufumbuzi akinifu dhidi ya changamoto zinazoikabili sekta ya wachezaji katika Afrika.
Warsha iliyoendeshwa chini ya uenyekiti wa Firdoze Bulbulia, ilihudhuriwa na wasemaji mashuhuri kama Ayuko Babu ambaye ni mtaalam wa filamu za Afrika, Mahmoud Thabit Kombo, Mwenyekiti wa ZIFF, na Hannelie Bekker kutoka Zuku.
Akitoa maoni yake kuhusu kauli mbiu mbele ya jopo hiyo , Hannelie Bekker, ambaye anasimamia vituo saba (7) vya; Zuku, alisema “Zuku itakuwa na jukumu muhimu katika kupandisha viwango vya ubora wa filamu za kiafrika kwa sababu inatoa nafasi kwa watengenezaji wa filamu na wazalishaji kuuza na kuonyesha bidhaa zao. Aidha, Zuku hasa ina nia ya kukuuza vipaji vya ndani na kutangaza kazi za wasanii wa ndani – na huo ndio jukumu msingi wa uwekezaji wetu na uhusiano na ZIFF. Tunahitaji filamu na tamthilia zenye bora na hii ina maana tuna maslahi ndio maana tunataka kuona sekta hii ikistawi.”
Ayuko Babu, ambaye pia alikuwepo kwenye jopo, alisisitiza haja ya watengenezaji wa filamu kujipanga na kufanya kazi pamoja ili kuboresha hali ya sekta ya filamu. Aidha alisisitiza haja ya kusaidia na kuimarisha ZIFF. “Zanzibar ni mahali pazuri na kila mtu anaifahamu hivyo kwa hiyo kuna umuhimu kwa kila mtu kujua kuhusu hilo na ZIFF ina fursa ya kukua kama matamasha mengine ya kimataifa kama vile Cannes na Ouagadougou.” Pia alizitaka watengenezaji wa filamu kufikiri kwa makini kuhusu mifano ya biashara yao ili kuhakikisha kwamba wanapata faida na wanahakikisha kwamba wanawapa watu hadhithi zinazoleta manufaa.
Mwakilishi wa wacheza filamu, Farida Nyamachumbe alizungumza kuhusu changamoto alizokabiliana nazo ndani ya sekta.
Jambo ambalo liliwavutia sana wasanii wa ndani ambao changamoto ya udhibiti, uwekezaji na usambazaji ni sehemu yao ya kusaidia uwanda huu. Pamoja na changamoto hizo,Farida alisema anamatumaini katika ukuaji wa filamu za Bongo.
Mjadala huo ulihudhuriwa na watengenezaji wa filamu kutoka Rwanda, Afrika Kusini, Nigeria, Namibia, Kenya, Marekani, Sweden na wasanii wa filamu za Bongo.
Zuku ambayo ni kampuni ya TV ya kulipia ambayo inaendelea kukua kwa kasi inapatikana Tanzania, Uganda na Kenya, ina nia ya kudhamini ZiFF kwa kipindi cha miaka 10 kwa thamani ya jumla ya dola milioni moja.
Udhamini huo unatarajiwa kutoa utulivu na msaada ambayo kwa upande utachangia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha sekta ya filamu, si tu nchini Tanzania lakini maeneo mengine ya Afrika.
Kingamuzi cha Zuku kinatoa wigo mpana wa uchaguzi wa burudani ka vile habari za michezo, sinema, makala na muziki. Hizi ni pamoja na chaneli tatu za BBC World News, MTV Base, Setanta Sports, Fox Entertainment na E!. Zuku pia inatoa chanelli zingine kama Zuku AFrika, Zuku Life, Zuku Sports na Zuku Movies. Huduma hii patikana kupitia satellite mahali popote Tanzania