Mashambuliaji wa kiabu ya Paris St-Germain Zlatan Ibrahimovic ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 inakkwisha msimu huu na amehusishwa na uhamisho wa Manchester United,kilabu ya Los Angels Galaxy na AC Milan.
PSG imesema kuwa Ibrahimovic anaondoka kama mshambuliaji bora na mchezaji bora zaidi katika historia ya kilabu hiyo.
Ibrahimovic ameifungia mabao mengi zaidi klabu hiyo licha ya kujiunga nayo mwaka 2012, amefunga mabao 152 katika mechi 178.
PSG imeshinda taji la Ligue 1 kila msimu tangu Ibrahimovic ajiunge na kilabu hiyo.