Zitto Kabwe na Ziara ya CHADEMA Jimbo la Bukene, Nzega

img-20131011-wa0002

 

Zitto Akihutubia wanachadema na wapenzi wengine wa chama hicho.

img-20131011-wa0012

img-20131011-wa0016

 

Ufunguzi wa matawi mapya pia ni kazi ya timu hiyo.

img-20131011-wa0021

 

Wakati mwingine ni kutembea na wananchi

img-20131011-wa0027

 

Gari ya muheshimiwa inapo pata pacha lazima wote tushirikiane.

Na Zitto Kabwe

TIMU ya CHADEMA Kanda ya Magharibi ikijumuisha Mwenyekiti wa Kanda Ndg. Mambo na Wenyeviti wa Mikoa 3 ya Kigoma, Tabora na Katavi tumetembelea Jimbo la Bukene, wilaya ya Nzega.

Kama ilivyo kwa mikutano iliyopita tumezungumza umuhimu wa Katiba na mchakato wake kutopendelea chama chochote cha siasa kwani tunaandika katiba ya nchi, umuhimu wa mwafaka wa kitaifa na kuwapongeza viongozi wakuu wa vyama kwa kukubali kufanya mazungumzo ili kupata mwafaka.

Pia tuliwaambia wananchi wasikubali mbinu chafu za kutaka kuongeza muda wa Bunge mpaka 2017 kwani itakuwa ni kinyume na katiba yenyewe.

Wananchi wa Bukene ni wakulima wa Pamba na sehemu kidogo Tumbaku. Kioja tulichokikuta Bukene ni wananchi kuuziwa dawa za Pamba feki ambazo haziui wadudu! Wananchi wa vijijini wanafanyiwa kila aina ya dhulma na kukandamizwa.

Pia tulielezwa namna watendaji wa vijiji na kata wanavyonyanyasa raia kwa kujifanya wao wakamataji, waendesha mashtaka na mahakimu. Wanatoza faini wananchi kwa kesi za kubambika.

Itabidi tutafute namna ya kuhakikisha hatua zinachukuliwa dhidi ya watendaji wa kata na vijiji wanaokiuka misingi ya utawala bora. Wananchi wa vijijini wana haki ya kuishi kama raia wengine wa Tanzania. Tusiwasahau