Balozi wa Sweden Nchini, Lennarth Hjelmaker akisisitiza jambo mara ujumbe wa Sweden ulipofanya kikao na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja (Mb) kwenye ofisi za Wizara mapema leo mchana.
Waziri wa Biashara Sweden Dk. Ewa Bjȍrling akimkabidhi Waziri wa Nishati na Madini zawadi mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichoshirikisha ujumbe kutoka Sweden na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini. Nia ya ziara ya ujumbe huo ni kubaini fursa za uwekezaji nchini hususan katika nishati jadidifu (renewable energy), mawasiliano ya simu na mitambo.