
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba Maendeleo na Makazi, Goodluck Ole Medeye ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi akiweka jiwe la msingi katika darasa lililojengwa kwa msaada wa wafadhili toka Marekani kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya Maingi ya Oldonyowas iliyopo kata ya Oldonyosambu, wilayani Arumeru, Arusha juzi.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba Maendeleo na Makazi, Goodluck Ole Medeye akiwapa zawadi ya kimila wafadhili waliojenga darasa katika shule hiyo inayokabiliwa na tatizo la upungufu wa madarasa kutokana na wingi wa wanafunzi ambapo kuna madarasa 7 wakati mahitaji yakiwa ni madarasa 12.