Ziara ya Kikazi ya Rais Kikwete Nchini Canada

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper katika jengo la Bunge la Seneti la nchi hiyo, ambapo viongozi hayo wawili walifanya mazungumzo Alhamisi Oktoba 4, 2012

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper wakishudia uwekaji sahihi mkataba wa ushirikiano kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Mhe. Bernard Membe na Waziri wa Canada katika Bunge la seneti la nchi hiyo Alhamisi Oktoba 4, 2012

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti katika bustani ya Jumba la Rideau Hall jijini Ottawa katika siku ya pili ya ziara yake rasmi nchini Canada huku akishuhudiwa na Gavana Jenerali wa nchi hiyo Mhe David Johnson na mkewe Mama Sharon Johnson Alhamisi Oktoba 4, 2012

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Spika wa Bunge la Seneti la Canada ramani ya dunia na njia za meli, pamoja na kuoneshwa chemba ya mikutano ya Maseneta wa Bunge la Canada Alhamisi Oktoba 4, 2012

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mabalozi wa nchi za Afrika wanaowakilisha nchi zao nchini Canada, na baadaye kupiga nao picha ya pamoja. (Picha Zote na Ikulu)