CHAMA cha Soka Zanzibar (ZFA) kimewafungia wachezaji wake wote waliokuwa katika kikosi cha timu ya taifa (Zanzibar Heroes) ambao walikuwa wakishiriki michuano ya CECAFA Tusker Chalenji. Wachezaji hao wamefungiwa kucheza soka ndani na nje ya nchi na kutakiwa kurejesha fedha zote za zawadi ya Dola 10000 za msindi wa tatu walizopokea nchini Uganda na kuamua kugawana wenyewe bila kushirikisha uongozi.
Kwa mujibu wa taarifa ya ZFA waliofungiwa ni:- makipa; Mwadini Ali (Azam), Suleiman Hamad (Black Sella), Abdalla Juma (Kipanga), mabeki; Nassor Masoud ‘Chollo’ (Simba), Samir Haji Nuhu (Azam), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub Ali ‘Canavaro’ (Yanga), Aziz Said Ali (Kmkm), Mohammed Juma Azan (JKU) na Ali Mohammed Seif (Mtende Rangers).
Wengine ni viungo; Hamad Mshamata (Chuoni), Ali Bakar (Mtende Rangers), Is-haka Mohammed (JKU), Twaha Mohammed(Mtibwa Sugar), Suleiman Kassim ‘Selembe’ (Coastal Union), Saad Ali Makame (Zanzibar All Stars), Makame Gozi (Zimamoto), Issa Othman Ali (Miembeni), Aleyuu Saleh (Black Sella), Khamis Mcha Khamis ‘Viali’ (Azam) na washambuliaji; Amir Hamad (JKT Oljoro), Jaku Juma Jaku (Mafunzo), Abdallah Othman (Jamhuri), Nassor Juma (JKU) na Faki Mwalim (Chipukizi).