Na Mwandishi Wetu
TIMU ya Zanzibar, imeshindwa kutumia fursa ya kucheza nyumbani huku ikishangilia na idadi kubwa ya mashabiki na wapenzi wa mpira wa miguu jijini Dar es Salaam.
Zanzibar ambayo katika mchezo wake wa kwanza iliupoteza leo imeshindwa kutamba dhidi ya vijana wa Burundi baada ya kutoka sulu ya bila kufungana hadi dakika 90 zinamalizika.
Akizungumza mara baada ya mchezo, Kocha Mkuu wa vijana wa Zanzibar, Abdul Fatah Abass amesema wamecheza vizuri lakini wameshindwa kutumia nafasi walizozipata.
Hata hivyo ametamba kuwa bado wana nafasi ya kufanya vizuri katika mechi yao ya mwisho dhidi ya vibonde Somalia. Mchezo ya kesho yote ni migumu, ambapo Somalia inacheza na Uganda, Kenya na Malawi na Wasudani watapepetana na Ethiopia.