Waziri wa Habari Vijana na Utamaduni Dk. Emmanuel Nchimbi akimkabidhi kombe na Fedha taslimu sh. milioni 3 nahodha wa timu ya Habari kutoka Zanzbar Bi. Mwanaidi Awadhi mara baada ya timu hiyo kuibuka na ushindi kwa kushika nafasi ya kwanza kwenye mchezo wa mpira wa pete kwa wanawake katika mashindano ya 9 ya NSSF kwa vyombo vya habari Machi Mosi, 2012 jijini Dar es Salaam. Timu hiyo imeifunga timu ya wanawake ya TBC queens kwa jumla ya magori 30 kwa 10. Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.
Kikosi cha timu ya mpira wa miguu cha Habari kutoka Zanzbar kikishangilia ushindi mara baada ya kutwaa kombe na fedha taslimu shilingi milioni 3.5 mara baada ya kuwaondoa wenyeji wa mashindano hayo timu ya NSSF kwa bao 4-0 Machi Mosi, 2012 jijini Dar es Salaam. Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.
Nahodha wa Timu ya TBC queens Bi. Grace Kingalame (kulia) akipokea zawadi ya mshindi wa pili kwa niaba ya timu yake sh. milioni 2 na kombe kutoka kwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya NSSF kwa vyombo vya habari Machi Mosi, 2012 jijini Dar es Salaam. Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.
Nahodha wa timu ya TBC queens Grace Kingalame(kulia) akionyesha ujirani mwema kwa kushangilia na wachezaji wa timu ya wanawake ya mpira wa pete ya Habari kutoka Zanzbar licha ya timu hiyo kuifunga TBC queens magori 30 kwa 10 Machi Mosi, 2012 jijini Dar es Salaam. Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.