Zanzibar, jina kubwa!

Bango la Zanzibar Club ndani ya Santa Monica, California

Na Rungwe Jr.

Watanzania tunazidi kufarijika tunapoona majina ya nchi zetu yanatumika maeneo haya ya ughaibuni, kwa watu kufanya biashara na kujikimu maisha yao. Pamoja na hayo ndugu zangu, hii ni changamoto kwetu wote! Kwani Club kama hii si ingekuwa poa sana kama ingemilikiwa na Mtanzania au Mzanzibar?. Habari ambazo TheHabari haikuweza kuthibitisha mara moja, ni kwamba Club hii ina milikiwa na Mkameruni. Tutafika tu, ipo siku ndani ya California kutakuwa na ‘Club Temeke’, ‘Club Gongo la Mboto’, ‘Club Kigamboni’ na kadhalika….

Bango la Club Zanzibar likionyesha mambo yalivyo kuanzia Jumatatu hadi Jumapili.

Club Zanzibar kama inavyoonekana kwenye kona.

Magari yakiwa yameegeshwa karibu na Club Zanzibar

Mlango wa kuingilia Club Zanzibar