ZADIA Yaunga Mkono Msimamo wa Kizalendo

zadia

Akizungumza kwenye kongamano maalum huko Zanzibar, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Massoud Othman alielezea wajibu wa kila Mzanzabari wa kuutetea umoja wa Wazanzibar.
Akifafanua kifungu cha 23 cha Katiba ya Zanzibar, Bw. Othman alielezea kuwa, mbali na Katiba hiyo kutoa haki sawa kwa Wazanzibari wote, pia inatoa wajibu kwa wananchi.
Miongoni mwa wajibu wa kila Mzanzibari kwa mujibu wa Kifungu hicho, ni wajibu wa kulinda, kuhifadhi na kudumisha Uhuru wa Zanzibar, Mamlaka ya Zanzibar, Ardhi ya Zanzibar na Umoja wa Zanzibar.
Maelezo hayo ya Mheshimwia Othman, yanakwenda sambamba na malengo makuu ya Jumuiya ya Wazanzibari waishio nchini Marekani (ZADIA).
Kwa hivyo, ZADIA inapenda kuchukua fursa hii kumpongeza na kumuunga mkono Mheshimiwa Othman Massoud Othman kwa kauli zake hizo za kizalendo alizozitoa tarehe10/10/215 mjini Unguja.

Bwana Othman alikumbusha jinsi alivyotekeleza wajibu wake huo wa kikatiba kivitendo kwa kupiga kura “kama alivyopiga” kwenye Bunge Maalum la Katiba kule Dodoma.

Aidha, alifafanua kasoro zilizomo kwenye Katiba pendekezwa ya Tanzania ambazo alizielezea kuwa hazina maslahi kwa Zanzibar.
Kitendo hicho cha kijasiri, na maelezo hayo, vinatoa changamoto kwa Kila Mzanzibari kuiga mfano huo. Nasi Wanadiaspora tumezipokea kwa moyo wote changamoto hizo na kuzifanyia kazi kama ambavyo imekuwa kawaida yetu. Natutafanya juhudi zote na tutashirikiana na wadau wote, ili kuhakikisha kuwa Zanzibar inapata hadhi yake na haki zake ndani ya Muungano wa Tanzania.