YANGA SC tayari imewasili mjini Antalya, Uturuki kwa kambi ya siku tano kujiandaa na mchezo wake wa pili wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe ya DRC mwishoni mwa wiki Dar es Salaam.
Yanga imefikia katika hoteli ya Rui, ambako pia waliweka kambi kabla ya mchezo wao wa kwanza wa kundi hilo dhidi ya Mouloudia Olympique Bejaia.
Ikumbukwe Yanga SC ilianza vibaya mechi za Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya kufungwa bao 1-0 wenyeji Mouloudia Olympique Bejaia Uwanja wa Unite Maghrebine mjini Bejaia Jumapili.
Kikosi kamili cha Yanga kilichopo kambini Uturuki ni makipa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Deo Munishi ‘Dida’ na Benno Kakolanya.
Mabeki; Hassan Kessy, Mwinyi Haji, Oscar Joshua, Andrew Vincent ‘Dante’, Mbuyu Twite, Kevin Yondan, Pato Ngonyani, Vincent Bossou na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Viungo; Thabani Kamusoko, Juma Mahadhi, Said Juma ‘Makapu’, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Godfrey Mwashiuya na Obrey Chirwa.
Washambuliaji; Donald Ngoma, Matheo Anthony na Amissi Tambwe.
Msafara upo chini ya Kocha Mkuu, Mholanzi, Hans van der Pluijm, Kocha Msaidizi Juma Mwambusi, Kocha wa makipa, Juma Pondamali, Daktari Edward Bavu, Mchua Misuli, Jacob Onyango, Mtunza Vifaa Mohammed Mpogolo na Meneja Hafidh Saleh.
Chanzo: Binzubeiry.co.tz