Klabu ya Yanga imekuwa ya kwanza kufuzu kucheza robo fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cu (ASFC) baada ya jana kuichapa JKT Mlale ya Ruvuma kwa bao 2-1 kwenye uwanja wa taifa.
Mlale ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 22 kipindi cha kwanza kupitia kwa mchezaji Shabani Mgandila aliyefunga goli hilo kwa uwezo mkubwa baada ya safu ya ulinzi ya Yanga kufanya makosa.
Yanga ilikuja juu na kusawazisha bao hilo mfungaji akiwa ni Paul Nonga aliyeunganisha pasi ya Geofrey Mwashiuya dakika ya 38 kipindi cha kwanza.