Na shaffihauda.com
Yanga imefanikiwa kuiondosha timun ya Cercle de Joachim ya Mauritius kwa jumla ya bao 3-0 baada ya leo kuichapa kwa bao 2-0 kwenye mchezo wa marudiano uliochezwa kwenye uwanja wa taifa.
Amis Tambwe alikuwa wa kwanza kuipa Yanga bao la kuongoza dakika ya 4 kipindi cha kwanza kabla ya Thabani Kamuso kupasia kamba dakika ya 55 kipindi cha pili na kuipa Yanga ushindi huo wa michuano ya kombe la klabu bingwa Afrika.
Ushindi huo unaipeleka Yanga kwenye hatua ya pili ya michuano ya ligi ya mabingwa Afrika ambapo itakutana na APR ya Rwanda katika hatua inayofuata.
Unachostahili kujua
Malimi Busungu, Geofrey Mwashiuya na Mwinyi Haji leo walikuwa wanacheza mchezo wa klabu bingwa barani Afrika kwa mara ya kwanza.
Yanga imefanikiwa kushinda michezo miwili ya hatua ya awali kwenye michuano hiyo dhidi ya Cercle de Joachim. Mchezo wa kwanza Yanga ilishinda kwa bao 1-0 ugenini kabla ya leo kushinda kwa bao 2-0 kwenye uwanja wa taifa.
Yanga inakutana kwenye raundi ya pili kwenye michuano ya Afrika dhidi ya timu ya Afrika Mashariki. Msimu uloiopita wakati ikicheza kombe la shirikisho Yanga ilicheza dhidi ya BDF ya Botswana katika hatua ya awali, ikacheza dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe kabla ya kuondoshwa na Etoile du Sahel ya Misri.
Yanga imeishinda Azam FC ambayo msimu uliopita iliondoshwa kwenye hatua ya awali na El Meirekh ya Sudan. Yanga imefuzu kwa hatua inayofuata baada ya kushinda michezo yake yote miwili ya hatua ya awali.
APR ambayo inakutana na Yanga kwenye raundi ijayo ya michuano hiyo, imeshinda mechi yake ya leo kwa magoli 4-1 dhidi ya Mbabane kwenye jijini Kigali.
Yanga itaifuata APR jijini Kigali, Rwanda kukipiga mchezo wa kwanza mapema mwezi ujao huku mechi ya marudiano ikipigwa jijini Dar es Salaam.