Yanga yaingia Robo Fainali Kagame Cup


Kikosi cha timu ya Yanga

GOLI la mshambuliaji, Davies Mwape wa Yanga limeivusha timu hiyo katika hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Kombe la Kagame inayoendelea Tanzania kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Mwape aliandika goli hilo kwa Yanga kwa shuti kali kutoka katikati ya uwanja ikiwa imesalia dakika moja ya nyongeza. Hata hivyo awali kadri muda ulivyokuwa ukiyoyoma ndiyo mashabiki wa Yanga walivyokuwa wakikata tamaa baada ya timu yao kutoka sare ya mabao 2-2 na timu ya Bunamwaya katika muda wa kawaida.

Mchezo huo uliokuwa ukitegua kitendawili nani ataingia hatua hiyo ulikuwa mzuri kwa kila timu kufanya mashabulizi makali katika lango la mwewnzake. Dalili za Yanga kuingia hatu hiyo zilianza kuonekana dakika ya 5 ya mchezo baada ya mchezaji, Rashid Gumbo kukosa goli la wazi akiwa na kipa wa timu ya Bunamwaya.

Dakika ya 26 ya Mchezo baada ya mchezaji Hamis Kiiza kuipatia timu yake goli la kwanza baada ya kazi nzuri ya Shadrack Nsajigwa aliyepiga krosi nzuri naye kuukwamisha wavuni. Mchezaji Rashid Gumbo aliiakikishia timu yake kuingia hatua hiyo baada ya kuifungia goli la pili baada ya kupiga shuti kali akiwa mita 30 na kutinga wavuni.
Goli la Bunamwaya limefungwa na Kasule Owen baada ya kupata pasi safi toka kwa Ssali Edward goli hilo liliamsha vifijo na nderemo kwa mashabiki wa Simba ambao muda mwingi walionekana kunyamaza kutokana na kikosi cha Yanga kucheza mpira mzuri.
Baada ya kupata goli la kwanza Bunamwanya waliongeza mashambulizi na kusawazisha goli la pili kupitia kwa mchezaji Kasule Owen katika dakika ya 75 akiunga vyema mpira uliochongwa na mchezaji Odur Tonny.

Mwamuzi Kirwa Sylivester toka Kenya alimpa kadi ya Njano mchezaji wa Yanga Davies Mwape, baada ya kumchezea vibaya Seku Ronald, Nsajigwa alipaata kadi ya njano alicheza vibaya mchezaji wa Bunamwaya.

Katika dakika ya 70 mpaka 87 kikosi cha Bunamwaya kilionekana kuutawala mchezo huo ikiwa ni pamoja na kupata nguvu kwa kushangiliwa kwa nguvu na mashabiki wa Simba. Katika hali isiyo ya kawaida mashabiki walikuwa wakishangilia ccm ccm pale yanga ilipokuwa wakishindwa kuumiliki mchezo. Katika mchezo wa Elman na El Mereikh ilipata magoli kupitia kwa Mohamed Mugadam Mohamed Fido dakika ya 51 na 57.

YANGA- Yaw Berko, Shadrack Nsajigwa/Julius Mrope, Geofrey Taita, Oscer Joshua, Chacha Marwa, Nurdin Bakar, Bakar Mbegu, Rashid Gumbo, Davies Mwape, Hamis Kiiza na Kiggi Makasi/Keneth Asamoah.

BUNAMWAYA – Muwonge Hamza, Kisakiita Robert. Kavuma Habib, Seku Ronald, Ssal Edward, Muganga Ronald, Kasule Owen, Ssali Andy/Mutyaba Mike, Odur Tonny na Luwaga Kizito/Bukenye Deus.

CHANZO; Jambo Leo.