Yanga yachezea kichapo tena, Simba yatafuna tena

Kombe la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania

Na Mwandishi Wetu

TIMU ya Yanga ya Dar es Salaam jana imeendelea kuanza vibaya Ligi Kuu ya Vodacom baada ya kujikuta ikifungwa tena na Timu ya JKT Ruvu kwa bao moja kwa mtungi. Yanga ambayo jana mjini Morogoro ilionekana kucheza kwa kuzidia karibuni muda wote wa mchezo, ilijikuta ikifungwa goli moja kwa njia ya penati baada ya mmoja wa washambuliaji wa JKT kufanyiwa mazambi kwenye eneo la hatari. Mchezaji Kessy Mapande wa JKT ndiye aliyepeleka kilio kwa Yanga baada ya kufunga penati hiyo.
Hadi mwisho wa mchezo Yanga 0 na JKT Ruvu 1.
Wakati huo huo Simba ya Dar es Salaam imeendelea kuanza vizuri ligi hiyo baada ya kuifunga JKT Oljoro mabao 2 kwa 0, katika mchezo huo ulipigwa mkoani Arusha Simba walionekana kuutawala mchezo tangua awali, hivyo hadi mwisho wa mchezo Simba 2 na JKT Oljoro sifuri.