Yanga Simba Chali Mapinduzi Cup, Mtibwa Akabidhiwa URA

PicsArt_1452436710582

YANGA SC imeaga michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kufungwa na URA ya Uganda kwa penalti 4-3, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90.

Penalti za Yanga zilifungwa na Kevin Yondan, Deo Munishi ‘Dida’ na Simon Msuva huku Malimi Busungu na Geoffrey Mwashiuya wakikosa, wakati za URA zimefungwa na Deo Othieno, Said Kyeyune, Jimmy Kulaba na Brian Bwete, wakati Sam Sekito alikosa.

Awali ndani ya dakika 90, Yanga SC walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na mshambuliaji Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe.
Tambwe alifunga bao hilo dakika ya 13 kwa kichwa akimalizia mpira uliorudi baada ya kutemwa na kipa wa URA, Brian Bwete kufuatia mchomo wa winga Simon Msuva.

yanga

Yanga ingeweza kumaliza dakika 45 za kwanza inaongoza kwa mabao zaidi kama si wachezaji wake kupoteza nafasi za wazi.
katika mastaajabu ya wengi alipiga juu na kuharibu krosi nzuri ya Msuva dakika ya 15.
URA nao walipoteza nafasi dakika ya 18 kupitia kwa mshambuliaji wao, Elkannah Nkugwa aliyepiga pembeni mpira na kuharibu pasi aliyopewa na Said Kyeyune.

Kipa wa URA aliinyima tena Yanga nafasi ya kufunga baada ya kudaka shuti lililopigwa na Tambwe aliyemalizia pasi ya kiungo stadi, Thabani Kamusoko dakika ya 38.
Kipindi cha pili, URA walikuja kivingine na kufanikiwa kusawazisha bao hilo kupitia kwa Peter Lwasa dakika ya Dk 76 baada ya makosa ya safu ya ulinzi ya Yanga.

Baada ya bao, hilo Yanga SC waliongeza kasi ya mashambulizi kwenye lango la URA kusaka ushindi, lakini hawakufanikiwa hadi walipokwenda kufia kwenye mikwaju ya penalti.

Nayo Simba ilijikuta ikipokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Mtibwa Sugar na kuaga mashindano ya kombe la Mapinduzi katika mchezo wa mapema.

PicsArt_1452436974603

Nyota wa Mtibwa iliyokuwa bora uwanjani alikuwa Ibrahim Jeba aliyefunga bao safi katika dakika ya 45 akitumia vizuri uzembe wa kipa wa Simba, Manyika Peter aliyeshindwa kuficha shuti la Shiza Kichuya na kupangua kizembe mbele ya Jeba.

Simba licha ya kucheza na viungo wanne Justice Majabvi, Awadhi Juma, Jonas Mkude na Mwinyi Kazimoto ilishindwa kucheza soka la kivutia katika dakika 80 za mchezo na kuonekana hatari katika dakika 10 za mwisho. Viungo wa Mtibwa wakiongozwa na mkongwe, Shaban Nditi walifanikiwa kulikamata dimba la kati kisawasawa mbele ya viungo hao ghali zaidi nchini.

Mabeki wa Simba, Juuko Murshid, Hassan Isihaka na Mohamed Hussein walionekana kama hawako mchezoni na kufanya makosa ya mara kwa mara na kama wachezaji wa Mtibwa wangekuwa makini wangeweza kupata mabao mengi zaidi.

URA sasa itakutana na Mtibwa Sugar iliyoitoa Simba SC kwa kuifunga bao 1-0 katika fainali Jumatano Uwanja wa Amaan, wakati Yanga inarejea Dar es Salaam.