Yanga Sc Yanusa Ubingwa, Azam Yaishusha Simba

yanga

YANGA SC imetanua kwigo kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mgambo JKT jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ushindi huo unaifanya Yanga ifikishe pointi 62 baada ya kucheza mechi 25, ikifuatiwa na Azam FC sasa yenye pointi 58 za mechi 25 pia, wakati Simba SC inaendelea kushika nafasi ya tatu kwa pointi zake 57 za mechi 25.

Bolly Shaibu aliifungia Mgambo JKT dakika ya nne, akimalizia pasi ya Nassor Gumbo ambaye alimpokonya mpira kiungo wa Yanga, Salum Telela nje kidogo ya boksi baada ya kuanzishiwa na kipa wake, Deo Munishi ‘Dida’.

Kiungo Deus Kaseke akaifungia Yanga bao la kusawazisha dakika ya 43 akimalizia pasi ya kichwa ya Mrundi Amissi Tambwe baada ya krosi nzuri ya juu ya beki wa kushoto, Oscar Joshua na Deus Kaseke tena akawainua vitini wana Yanga dakika ya 72

AZAM-FC_01

Nao Azam FC imeipiga kumbo Simba SC katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 2-0 jioni ya leo dhidi ya Majimaji ya SOngea Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Shujaa wa Azam FC leo alikuwa ni kiungo Mudathir Yahya Abbas aliyefunga mabao yote mawili kipindi cha pili, dakika ya 51 na 63.
Azam FC sasa pointi 58 baada ya kucheza mechi 25 za Ligi Kuu na kupanda hadi nafasi ya pili, nyuma ya mabingwa watetezi, Yanga yenye pointi 62 za mechi 25 pia, ikiiteremshia Simba yenye pointi 57 za mechi 25 pia nafasi ya tatu

Chanzo: Bin zubeiry.co.tz