Yanga Noma, Yaichinja Simba Tena…!

Adbi Banda akiwaungia mkono mashabiki wa Simba mara bada ya kutolewa nje ya mchezo kwa kadi nyekundu na mwamuzi Jonesi Rukyaa kufuatia kuoneshwa kadi mbili za njano. (Picha kwa hisani ya Shafii Dauda Blog)

Adbi Banda akiwaungia mkono mashabiki wa Simba mara bada ya kutolewa nje ya mchezo kwa kadi nyekundu na mwamuzi Jonesi Rukyaa kufuatia kuoneshwa kadi mbili za njano. (Picha kwa hisani ya Shafii Dauda Blog)

TIMU ya Yanga leo imefanikiwa kutamba tena kwa watani wao wa jadi baada ya kuibamiza timu ya Simba mabao 2-0 huu ukiwa ni mchezo wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Yanga katika mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa walifanikiwa kupata bao la kwanza katika dakika ya 39 ya kipindi cha kwanza mfungaji akiwa ni Donald Ngoma aliyetumia makosa ya Hassan Kessy wa Simba kutoa pasi fupi kwa golikipa wake Vicent Agban na kunaswa na mfugaji wa goli.

Kifo cha Simba kilihitimishwa na mchezaji wao wa zamani Amis Tambwe (kwa sasa anachezea Yanga) katika dakika ya 72 kipindi cha pili baada ya kufunga bao la pili la Yanga. Hadi mpira unamalizika ubao wa matokeo wa uwanja wa taifa ulisomeka Simba 0 na Yanga 2. Ushindi huo ni wa pili kwa Yanga dhidi ya Simba ndani ya msimu wa 2025-16 baada ya awali kupata ushindi kama huo kwenye mchezo wa raundi ya kwanza mwaka jana.

Hata hivyo katika mchezo huo Simba ililazimika kucheza pungufu ya mchezaji mmoja kwa zaidi ya dakika 66 baada ya mchezaji wake mmoja mlizi wa kati kuzawadiwa kadi mbili za njano na hatimaye nyekundu kwa mchezo mbaya ambao uliigharimu timu yake.

Matokeo ya michezo mingine iliyochezwa leo kwenye viwanja mbalimbali; ni kwamba timu ya Mgambo JKT imetoshana nguvu kwa magili 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons, huku Timu ya Stand United ikitoka suluhu ya 1-1 na timu ya JKT Ruvu. Timu ya Mbeya City wao wamelala kwa Azam FC baada ya kupigwa goli tatu kwa mtungi, huku timu ya Toto Africans ikitoka suluhu ya 1-1 na timu ya Kagera Sugar.