Kocha Mkuu wa Simba, Jackson Mayanja ameamua kikosi chake kuwa kinapata dozi moja tu kwa siku.
Uamuzi huo wa Mayanja ni wakati wa maandalizi ya mwisho ya Simba kabla ya kuivaa Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kesho.
“Sasa tunafanya mazoezi mara moja tu kwa siku, kocha amepitisha hilo. Nafikiri kila tunavyokaribia mechi na ukali wa mazoezi unapungua,” alisema mmoja wa wachezaji wa Simba ambaye hataki kutajwa jina.
Simba imeweka kambi mjini Morogoro kujiandaa na mechi hiyo inayotarajia kuwa ngumu kwa kila upande.
Nayo Yanga ipo kambini mjini Pemba kujiandaa na mechi hiyo pia na lengo kuu ni kuishinda Simba na kurejea kileleni.
Benchi la ufundi la Yanga sasa limeamua kufanya mazoezi ya siri bila ya wengine kuona nini kinachoendelea.
Yanga ipo kambini mjini hapa kujiandaa na mechi yake ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba, kesho Jumamosi.
Kuanzia jana, Yanga imeamua mazoezi yake kuanzia hatua fulani kufanyika bila ya kuwepo kwa watu wengine wasio wahusika kwenye Uwanja wa Gombani,.
Mashabiki, hata Waandishi mbalimbali wa habari, wamefukuzwa katika mazoezi ya Yanga ili Kocha Hans van Der Pluijm aendelee na “mambo yake”.
Awali, siku mbili za mwanzo, mashabiki na waandishi walipewa nafasi ya kuona mazoezi hayo. Lakini kuanzia juzi, mazoezi mwanzoni wanaweza kuruhusiwa lakini baada ya muda watu hutakiwa kutoka nje ya uwanja.
Habari na Binzubeiry.com