Woods Kurejea Kwa Kishindo Dimbani

Tiger_college
Mwanamichezo nguli aliyewahi kuwa mcheza golf namba moja duniani Tiger Woods, amesema kwamba ana matarajio ya kushinda michuano mikubwa zaidi katika kipindi cha miaka kumi ijayo.

Woods, ambaye mwishoni mwa mwezi huu atatimiza umri wa miaka 40, Woods amezidi kusuka katika nafasi za ubora wa mchezo huo

Tiger alifanyiwa upasuaji wa mgongo mwezi September mwaka huu hiyo ikiwa ni mara ya pili katika kipindi cha miezi 18 lakini ana matarajio ya kucheza kwa ufanisi zaidi mwanzoni mwa mwaka mpya wa 2016.

Woods amejiwekea rekodi ya kushinda katika mchezo wa golfu kwa wiki mia sita themanini na tatu kama bingwa wa dunia katika mchezo huo lakini alipoulizwa kuwa anaingia katika muongo wa tano akiwa na umri mkubwa , Tiger alijibu suala hilo kwa kusema kwamba “kiakili watu wanaonifahamu, wananijua kama kijana mdogo mwenye miaka mitano”.