WLAC Waibuka na Mabonanza Kupinga Ukatili wa Kijinsia

Mwanasheria wa Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake na Watoto (WLAC) Abia Richard, akizungumza wakati wa Tamasha la Vijana la kupinga Ukatili wa Kijinsia lililofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Picha na Nasma Mafoto.

Na Karama Kenyunko

KITUO cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake (WLAC), kimeanzisha bonanza maalum la michezo kwa ajili ya kuhamasisha jamii kupinga ukatili wa kijinsia. Bonanza hilo, limefunguliwa na mratibu wa WLAC, Abia Richard jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Bonanza hilo uliofanyika Mwembe Yanga, Temek, Abia amesema lengo la kuanzishwakwa bonanza hilo ni kutaka kuwaunganisha watanzania kupambana na vitendo hivyo vya ukatili wa kijinsia.

Amesema, katika kampeni nyingine ambazo wamekuwa wakiendesha, kundi kubwa ambalo limekuwa likihamasika ni wanawake na wasichana kwa hiyo wanaamini kuanzisha kampeni hiyo kutasaidia kuwahamasisha na wanaume.
Ameongeza, kati ya kundi linalotajwa katika kutenda vitendo vya ukatili wa kijinsia na wanaume pia wamo, lakini katika kampeni nyingi zinazoendeshwa za kuhamasisha kupambana na vitendo hivi, kundi la wanaume wamekuwa wakijiweka pembeni.

” Tunaamini katika kampeni hii kupitia bonanza, wanaume watashiriki kwa wingi kwa sababu wanapenda michezo,” amesema Abia.

Ameongeza kuwa, vitendo vya ukatili wa kijinsia vinapaswa kupambanwa na kila mtu katika jamii kwa kuwa vinaathiri sana jamii yetu. Wanaume hawapaswi kukaa pembeni, tunawaomba kupitia michezo hii nao washiriki kupambana navyo. Katika kampeni hiyo michezo mbalimbali imepangwa, kuwamp ikiwemo ya mpira wa miguu, pete, na mingine mingi, itakayowapa fursa na wanaume kushiriki.

Pia alisema wanatarajia kuanzisha timu baina ya madereva wa boda boda, bajaji na za vijana kutoka sehemu mbalimbali kwa ajili ya kuwahamasisha kuelimisha jamii kupinga vitendo hivyo. Katika uzinduzi wa kampeni  hiyo, timu ya mpira ya wanawake ya Simba gueen na Mburahati queen zote za jijini Dar es Salaam, zilimenyana na kutoka sare ya bila kufungana.

Wachezaji wa timu za Simba Queens na Mburahati Queens, wakichuana kuwani mpira wakati wa mchezo wao kwenye Bonanza hilo. Katika mchezo huo Mburahati Queens, waliibuka washindi kwa mikwaju ya penati 4-2. Picha Zote na Nasma Mafoto Viongozi wakikagua timu kabla ya kuanza kwa mtanange wa Soka kwa upande wa wanaume.