Wizara ya Afya, UNDP Kuanzisha Mradi wa Kupunguza Taka

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

 

Na Ally Daud, Maelezo – Dar es Salaam

HOSPITALI za Muhimbili, Amana, Mwananyamala na Kairuki za Jijini Dar es Salaam zinatarajia kuwekwa kwenye mradi maalum wa kudhibiti taka hatarishi ikiwa ni mkakati wa Serikali wa kuboresha usafi wa mazingira katika huduma za afya nchini.

Mradi huo wa kudhibiti taka hatarishi ikiwemo sindano, gloves, nyembe na bandeji unasimamiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mazingira uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma ya Afya na Kinga kutoka Wizara ya Afya, Dk. Neema Rusibawengile alisema kuwa lengo la mradi huo una lengo la kukabiliana na magonjwa ya maambukizi katika maeneo ya hospitali nchini.

“Mkutano huu umelenga kuandaa na mradi utaodhibiti taka hatarishi amabao utanza kufanya kazi katika hospitali za Muhimbili, Amana, Mwananyamala kairuki na baadaye kuendelea nchi nzima,” alisema Dk. Rusibawengile.

Dk. Rusibawengile alisema kuwa mkutano huo pia umewakutanisha wadau mbalimbali wa Maendeleo na Mazingira watakaojadili mbinu mpya za kutunza mazingira kwa ajili ya kupeuka magonjwa ya maambukizi nchini yanayotokana na taka hatarishi.

Kwa mujibu wa Dk. Rusibawengile alisema mkutano pia huo unalenga kupata njia mbadala za kupunguza uzalishaji wa mekyuri katika hospitali, zahanati na vituo vya afya ili kuondoa utumiaji wa vifaa vyenye nishati hiyo.

Kwa upande wa mratibu wa udhibiti wa taka hatarishi za Hospitali Dk. Honest Anicetus alisema wadau wa mkutano huo pia wamepanga kubuni mikakati ya kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya afya katika utunzaji wa mazingira.