Wito Kwa Kina Baba Kuondoa Dhana Potofu!

20140429-081853.jpg

20140429-081914.jpg

20140429-081930.jpg

20140429-081948.jpg

20140429-081958.jpg

20140429-082006.jpg

Maisha ya sasa kushirikiana kama picha zinavyoonyesha hapo juu, mke na mume kwakishirikiana kuuza vitumbua. Mke akichoma na mume akiwa anatoa huduma kwa wateja, ambao hujitokeza kwa wingi mida hii ya asubuhi pale maeneo ya “Davis Corner”, Tandika, Manispaa ya Temeke katika kituo cha daladala ziendazo Abiola na Buza kanisani.

Kitumbua kimoja huuzwa kwa Tsh 100, na awali kabla ya wanandoa hawa kuuza vitumbua, walikuwa wakijishughulisha na uuzaji wa Mihogo ya kukaanga. Mzee alikuwa akitengeneza chachandu na kachumbari, na mama alikuwa akikaanga mihogo. Ama kweli nguvu kijijini, mjini maarifa na akili.

Thehabari inatoa wito kwa wakina baba wote kuondoa fikra potofu kwamba kuuza vitafunwa ni kazi ya kina mama tu!

Picha Zote na Habari Kutoka kwa Mdau Wetu Maalum, Dar