Katika ligi ya Ungereza West Bromwich Albion katika mchezo ulioanza mapema imefanikiwa kuzoa pointi tatu baada ya kuilaza Wolves mabao 2-0 na kufanikiwa kupata ushindi wa kwanza wa nyumbani na kujikwamu eneo la kushuka daraja.
Chris Brunt alikuwa wa kwanza kuipatia West Brom bao la kuongoza baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Billy Jones.
Kevin Doyle naye alikaribia kuipatia bao Wolves na Roger Johnson akapoteza nafasi nzuri ya kufunga baada ya kupiga mpira kichwa uliotoka nje.
Lakini mchezaji wa akiba Peter Odemwingie aliipatia West Brom ushindi dakika za mwisho na kuifanya Wolves ipoteze mchezo wa tano mfululizo wa ligi.
Kwa matokeo West Brom imefikisha pointi nane na wapo nafasi ya 12.
-BBC