Danni Welbeck ambaye alikuwa anacheza mechi yake ya kwanza tangu Aprili mwaka uliopita ameifungia Arsenal bao la pili na la ushindi dhidi ya vinara wa ligi kuu ya Uingereza Leicester.
Welbeck alimhakikishia Wenger ushindi huo muhimu uliotamatisha msururu wa mechi 16 bila kushindwa wa kocha Claudio Ranieri.
Mchezaji mwengine wa akiba Theo Walcot ndiye aliyekuwa ameisawazishia Arsenal kunako dakika ya 70 ya kipindi cha pili.
Wageni hao ambao wamewashangaza wengi msimu huu kwa kufungua pengo la alama 4 kileleni mwa jedwali la ligi kuu ya Uingereza walikuwa wamefunga bao la kwanza kupitia kwa mkwaju wa penalti. Bao hilo lilitiwa kimiani na Jamie Vardy kunako dakika ya 45”.