Weka Mipaka Kwenye Ndoa Yako…!

20140117-120001.jpg

Na Ulindula:

UNAPOTEMBELEA sehemu mbalimbali utagundua kuwa kila nyumba nzuri yenye thamani imezungushiwa uzio, na uzio unaendana na thamani ya nyumba na vilivyomo. Utakuta nyingine uzio mrefu huwezi hata kuona miti iliyopo ndani na nyingine zipo wazi mtu yeyote anapita na kutoka kama anavyopenda. Vivyo hivyo ukiithamini ndoa yako utaiwekea mipaka, mipaka ambayo hakuna anayeweza kuivuka. Hapa simaanishi kumuwekea mwenzi wako mipaka, bali kuiwekea ndoa yako mipaka. Kila mwanandoa lazima ajiwekee mipaka. Mipaka hii itaiponya ndoa na wale wanaotaka ku tracepass na wewe itakusaidia pia kukulinda.

Wewe umeoa/ kuolewa ni kwanini basi unaruhusu mtu wa jinsia nyingine unayemuita rafiki yako akuzoee hadi kuvuka mipaka? Anakuwa huru kukushika na kukutania utani usiofaa na wewe unachekelea tu? Unakuta wafanyakazi ofisini wanashikana shikana na kutaniana na wapo kwenye ndoa, je huoni kama unaruhusu watu watracepass kwenye ndoa yako? Wengine hata kwenda lunch hawawezi bila dada au kaka fulani na wakati wapo kwenye ndoa.

Unapokuwa online unachat je umejiwekea mipaka? Message zako na jinsi unavyochat na watu umeweka mipaka? Watu wamejikuta wanatoka nje ya ndoa sababu ya ku entertain chat zisizofaa na hadi wanajikuta emotionally connected na mtu asiye mwenzi wake. Unafika nyumbani busy na simu na hata mwenzi wako huna muda naye tena maana tayari kuna mtu umeconnect naye emotionally kupitia simu.

Je ndugu wanaweza ingilia maamuzi yenu na kuyabadilisha bila nyie kuwasiliana? Ni nafasi gani wazazi wanayo kwenye ndoa yenu maana hapa pia panahitaji mipaka. Wazazi ni walezi na washauri lakini wenye maamuzi ni mume na mke.

Weka mipaka kwenye ndoa yako, tena mipaka inayostahili maana ndoa ina thamani kubwa!

Chanzo: Ulindula Brown Mwambela