Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta (kulia) akisalimiana na baadhi ya viongozi wa juu wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) baada ya kuwasili kiwanda cha kampuni hiyo cha jijini Dar es Salaam kutembelea kiwanda hicho.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Jaji Mstaafu, Mark Bomani (kushoto) akipewa taarifa fupi kwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ya utendaji wa Kampuni ya SBL na mchango wake katika kuliwezesha taifa kwa kodi na huduma za jamii.
Mkurugenzi wa Masoko wa Serengeti Breweries Ltd (SBL), Ephraim Mafuru kushoto akiwa kwenye kikao na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta alipotembelea kiwanda hicho leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Serengeti Breweries Ltd (SBL), Steve Gannon (kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta alipotembelea kiwanda hicho leo.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta akiwa katika kikao kifupi kati ya uongozi wa SBL alipotembelea kiwanda hicho leo kabla ya kuanza kuzunguka kuangalia utendaji wake.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akitembelea Kiwanda cha Serengeti Breweries Ltd Dar
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akitembelea Kiwanda cha Serengeti Breweries Ltd Dar
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akitembelea Kiwanda cha Serengeti Breweries Ltd Dar na kupata maelezo namna mitambo ya kiwanda hicho inavyofanya kazi kutoka kwa Meneja Ufungashaji wa SBL, Bw. Minja (aliyeshika bia).
Meneja Ufungashaji wa SBL, Bw. Minja (aliyeshika bia) akitoa maelezo namna idara yake inavyofanya kazi kwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta alipotembelea kiwanda hicho.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta akizungumza na vyombo anuai vya habari mara baada ya ziara yake alipotembelea kiwanda cha SBL cha jijini Dar es Salaam leo. Katika mazungumzo yake Waziri Sitta amekipongeza kiwanda hicho kwa namna kinavyofanya kazi kwa kuzingatia viwango na kutaka makampuni mengine kufuata staili hiyo. Amesema atazifikisha changamoto zinazokikabili kiwanda hicho Serikalini na kupitia idara husika wataangalia namna ya kupunguza urasimu katika ulinganifu na utambuzi wa viwango kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwani ni moja ya changamoto kwa SBL na wafanyabiashara wengine.