Waziri wa Fedha Tanzania, Mgimwa Katika Mazungumzo na Viongozi wa Benki ya Dunia

Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa akiwa na ujumbe katika mkutano, wa kwanza kulia ni Bi. Salome Sijaona ambaye ni Balozi nchini Japan akifuatiwa na Siyvacius B. Likwelile Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha akifuatiwa na Khamisi Mussa Omari Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Zanzibar katika mkutano Jijini Tokyo- Japan.

Ujumbe kutoka Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa pamoja na maofisa kutoka Benki ya Dunia wakiendelea na majadiliano juu ya kuangalia uwezekano wa kuisaidia Tanzania iweze kuendelea kiuchumi hapa Jijini Tokyo- Japan.

Waziri wa Fedha, Dk. Mgimwa akifafanua jambo kwa Ofisa wa Benki ya Dunia.

Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa akiwa pamoja na Gavana wa Benki Kuu, Benno Ndulu kwenye mkutano wa Mawaziri wa Afrika wakifuatilia mkutano wa Mawaziri wa Afrika ( Caucus meeting) ambapo majadiliano hayohuafikiwa kwa pamoja na kupelekwa ngazi za juu za uongozi wa IMF.Mkutano huo ulifanyika jijini Tokyo-Japan.

Viongozi wa Afrika wanaoongoza mkutano wa Mawaziri wa Afrika, Jijini Tokyo- Japan

Mawaziri wa Fedha wa Afrika katika mkutano wa pamoja wa Mawaziri Jijini Tokyo- Japan mkutano huo unajulikana kama (Caucus meeting). (Picha zote na Ingiahedi Mduma na Scola Malinga)

Mkutano wa ‘Caucus’ Wafanyika

Mikutano ya IMF inaendelea, wakati huo huo mikutano mingine ikichukua nafasi yake na kusaidia kujadili mambo ambayo yanaweza yakalisaidia Bara la Afrika. Mawaziri wa Fedha wa Afrika wakiambatana na Magavana wao wa Benki kuu leo wamehudhuria mkutano wa “CAUCUS”.

Mikutano hii inafanyika kwa lengo la kuwakutanisha Mawaziri wote wa Afrika ili kuweza kuzungumzia matatizo yao kwa ujumla na wakisha yakamilisha huyachambua na kuyapeleka kama ripoti moja kwa Rais wa Benki ya Dunia na kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimatafa.

Katika kikao hicho, Mawaziri hao wanazungumzia ni jinsi ni gani Taasisi hizo mbili zinavyoweza kuzitoa Nchi za Afrika na ni maeneo gani ambayo Afrika ikisaidiwa inaweza kuendelea.