Mh. Waziri wa Fedha Saada M. Salum(MB) akimsikiliza msimamizi wa duka la Salome Furniture wakati akijitetea baada ya kukutwa anafanya biashara bila ya kutumia mashine ya EFD.
Wafanyakazi wa Yono actions Marts ambao ni wakala wa TRA wakilifunga mojawapo la duka ambalo mmiliki wake aligundulika kufanya biashara bila ya kutoa risiti za mashine ya EFD.
Mh. Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum(MB) akitoa maelekezo kwa Meneja wa TRA mkoani Dodoma (mwenye miwani) na wakala wa TRA kutoka Yono Action Mart kulifunga duka la Salome Furniture baada ya kukutwa akifanya biashara bila ya kutumia risiti za mashine ya EFD.
Waziri wa Fedha Mh. Saada M. Salum(MB) akiwa katika mgahawa wa Dodoma Carnival alipotembelea kukagua matumizi ya mashine za EFD. Mh. Waziri aliagiza mgahawa huo ufungwe mpaka hapo watakaponunua mashine hizo. Kushoto kwa Mh. Waziri ni Meneja wa TRA Mkoa wa Dodoma na mwenye shati jekundu ni msimamizi wa mgahawa huo.
Mh. Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum(MB) akitoa maelekezo kwa Meneja wa TRA mkoani Dodoma (mwenye miwani) na wakala wa TRA kutoka Yono Action Mart kulifunga duka la Salome Furniture baada ya kukutwa akifanya biashara bila ya kutumia risiti za mashine ya EFD.
WAZIRI wa Fedha Saada Mkuya Salum amefanya ukaguzi wa ghafla katika baadhi ya maduka Mkoani Dodoma ili kuona kama maelekezo ya Serikali kuhusu matumizi ya mashine za EFD yanatekelezwa ipasavyo. Katika ukaguzi huo ambao ulihusisha maduka ya kuuza thamani za majumbani,nguo na maduka ya kuuza bidhaa mchanganyiko (Min supermarket), Waziri akiongozana na Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania aliagiza kufungwa kwa maduka yote ambayo yamekaidi agizo la Serikali la matumizi ya mashine EFD mpaka pale watakaponunua na kuzitumia ipasavyo mashine hizo.
Aidha Mh.Waziri amewataka wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kuisaidia Serikali kuwafichua wafanyabiashara wasio waaminifu na ambao wanapelekea kuikosesha Serikali mapato ambayo yangetumika katika kuboresha huduma za kijamii.