WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda Jumamosi, Machi 2, 2013 atakutana na Tume maalum aliyoiunda ili ifanye uchunguzi wa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne ambayo yalitangazwa Februari 18, mwaka huu. Mkutano huo utafanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni, jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3 asubuhi.
Tume hiyo inajumuisha wadau kutoka Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi (Tanzania Association of Managers and Owners of Non-Government Schools/Colleges (TAMONGSCO), Taasisi za Dini zinazotoa huduma ya elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Asasi zisizo za Kiserikali (NGOs) zinazoshughulikia masuala ya elimu.
Wadau wengine wanatoka Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA).
Katika matokeo hayo yaliyotangazwa Jumatatu wiki hii, asilimia 60 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne Oktoba, 2012 walifeli.