WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amekutana na Papa Francis wa Kwanza na kufanya naye mazungumzo ya faragha ikiwa ni pamoja na kuwasilisha salamu za pongezi kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete.
Waziri Mkuu alipata fursa hiyo jana mchana (Alhamisi, Machi 21, 2013) alipofika kwenye makazi ya muda ya Papa Francis wa kwanza kwenye hosteli ya Mt. Martha mara baada ya kumaliza vikao na wawakilishi kadhaa wa mashirika ya kimataifa walioko mjini Roma, Italia. Papa Francis anakaa hosteli kwa sababu Ikulu yake ilifungwa mara baada a Papa Benedict XVI kujiuzulu na sasa inafanyiwa ukarabati mdogo.
Alipowasili Vatican City, Waziri Mkuu alipokelewa na Mkuu wa Itifaki wa Baba Mtakatifu (Chief of Protocol of the Holy See) Monsinyori Jose Avelino Bettencourt ambaye pia alimtambulisha kwa Katibu Mkuu wa Baba Mtakatifu, Kardinali Tarcisio Bertone kabla hajaonana na Papa Francis wa Kwanza.
Katika mazungumzo yao, Waziri Mkuu alimweleza Papa Francis wa Kwanza kwamba amefika kuwasilisha salamu za pongezi kutoka kwa Rais Kikwete. Katika salamu hizo, Waziri Mkuu Pinda alisema: “Rais wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete anakutakia heri katika jukumu hili jipya ulilopewa na Mwenyezi Mungu. Tunamshukuru Mungu kwa kukupa jukumu la kulea wanakondoo, nasi tutaendelea kukuombea katika kazi yako kubwa uliyonayo.”
Waziri Mkuu alimweleza Papa Francis wa Kwanza kwamba Rais Kikwete alitamani kuwepo kwenye ibada yake ya kusimikwa rasmi lakini kutokana na majukumu mengine ya kitaifa aliyokuwa nayo, hakuweza kufika na badala yake amemuomba Waziri Mkuu amuwakilishe.
Akipokea salamu hizo, Papa Francis wa Kwanza alisema anatambua fika jinsi Tanzania inavyojitahidi kuendeleza amani chini ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete. “Tutaendeleza ushirikiano wa karibu uliokuwepo baina ya nchi zetu,” alimalizia Papa Francis wa Kwanza.
Mratibu wa Masoko wa Chuo cha Uandishi wa Habari School journalism Mass Communication (SJMC) Bi Sophia Ndibalema, akifafanua jambo kuhusiana na Udhamini wa Chuo hicho kwa Washiriki wa Miss Utalii Tanzania, walipotembelea chuo hicho kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali wakati wakijiandaa na Fainali za Taifa 2012/13.