chanzo millardiayo.com
Mbuzi 75 wakatwa mapanga na wengine kuuawa Mkoani Morogoro, Huku waziri wa mifugo, kilimo na uvuvi Mwigulu Nchemba akikasiliwa na Kitendo hicho cha Uvunjaji wa Sheria Inayolinda Mifugo
Leo February 9 2016 waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi Mwigulu Nchemba alilazimika kusafiri haraka hadi mkoani Morogoro kijiji cha Kambala wilaya ya Mvomero, baada ya taarifa za mapigano ya wakulima na wafugaji kumfikia.
Inasemekana zaidi ya mifugo 75 imeuawa kati ya mifugo 200 waliojeruhiwa kwa mapanga na silaha za jadi
Waziri Mwigulu amefika eneo la tukio na kuchukua hatua za haraka kwa kuagiza kamati ya ulinzi ya mkoa na wilaya, kufanya uchunguzi na kuwatafuta wahusika wa tukio la kukatwa katwa mapanga kwa zaidi ya mifugo 75 Ili wafike mbele ya mikono ya sheria nakuagiza mahakama kupitia upya hukumu iliyotolewa mwaka 2015 ya kugawa mipaka kati ya eneo la wakulima na wafugaji.
Mwisho waziri Nchemba ameagiza uongozi wa mkoa na wilaya kufanya mkutano wa hadhara wa wakulima na wafugaji tarehe 20/02/2016, ili kuanza harakati za kumaliza mgogoro. Kati ya mifugo inayotajwa ni mbuzi, kondoo na ndama.