Waziri wa Habari,Utamaduni,sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(katikati)akiongea na waandishi wa Habari na kuwaomba watanzania kumwombea Mbwana Samatta ili ashinde katika kinyanganyiro cha kugombea uchezaji bora wa afrika anayechezea ligi za ndani kwani ni jambo la Taifa zima.Mhe Nape pia alimhakikishia kuwa Serikali ipo nyuma yake na ipo katika mkakati wa kuifanya michezo kuwa Shughuli Rasmi kwani itawafaidisha wanamichezo na Serikali kwa kupata kodi.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo (kushoto) akifuatilia mahojiano kati ya waziri na waandishi wa habari (hayupo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa filamu ya HOMECOMING iliyozinduliwa jana jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrye Mungereza na Muandaaji wa filamu hii Bi. Seko Shamte. Picha na Frank Shija, WHUSM
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akimsikiliza Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo wakati wakiangalia filamu ya HOMECOMING wakati wa hafla ya uzinduzi wa filamu ya HOMECOMING jana jijini Dar es Salaam. Picha na Frank Shija, WHUSM
Mchezaji wa TP Mazembe Mbwana Samatta(wa kwanza kushoto)akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) sababu za yeye kumtembelea Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo katika ofisi ya Wizara hiyo.Mbwana alisema kuwa amemtembelea waziri uyo kwa ajili ya kumfahamisha kuwa yumo katika kinyanganyiro cha kugombea uchezaji bora wa afrika anayechezea ligi za ndani na hivyo kuomba baraka za Wizara.Pia kumpongeza Mhe. Nape kwa kuchaguliwa kuwa waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.Mbwana anategemea kujiunga na klabu ya Mpira ya Genk ya Ubelgiji kwa mkataba wa miaka minne.