Waziri Mkuu Mizengo Pinda akimweleza jambo Meneja wa Takwimu za Kilimo Bi. Joyce Urassa alipotembelea Ofisi ya Taifa ya Takwimu jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Ramani Ofisi ya Taifa ya Takwimu Vincent Mgaya (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuhusu matumizi ya ramani kupata Takwimu za Kilimo, Uchumi na Utalii.
Meneja wa Idara ya Pato la Taifa wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Daniel Mwasula akitoa ufafanuzi kwa Waziri mkuu Mizengo Pinda kuhusu Pato la Taifa na namna ofisi yao inavyofanya kazi kukokotoa pato la taifa.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa katika Picha ya Pamoja na viongozi na watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu mara baada ya kukamilisha ziara yake. Picha zote na Aron Msigwa – MAELEZO.