Waziri Mkuu Majaliwa Asafisha Soko Kariakoo, Viongozi Waitwa Kujieleza

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisafisha mtaro wa maji machafu kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam Desemba 9, 2015.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisafisha mtaro wa maji machafu kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam Desemba 9, 2015.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoka eneo la shimoni kwenye soko kuu la Kariakoo kufanya usafi Desemba 9, 2015. Kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoka eneo la shimoni kwenye soko kuu la Kariakoo kufanya usafi Desemba 9, 2015. Kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.


WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema zoezi la usafi lililofanyika leo nchini kote lisiishie hapo bali liwe endelevu ili Tanzania iwe na taswira nzuri kwa wageni wanaoingia nchini. Ametoa wito huo leo Desemba 9, 2015 sokoni Kariakoo wakati akishiriki zoezi la kufanya usafiikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli la kutaka maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru yasiwepo na badala yake watu wote washiriki kufanya usafi katika maeneo mbalimbali.

Waziri Mkuu Majaliwa pia amewataka viongozi wa soko la Kariakoo wafike ofisini kwake Desemba 14, 2015 saa 4 asubuhi ili wamueleze wana mikakati gani ya kuboresha utoaji huduma kwenye soko hilo. “Natambua kuwa siyo sahihi kupanga chini biashara tulizonazo. Nataka hawa viongozi waje wanieleze wana mpango gani endelevu wa kuboresha soko hili,” alisema Waziri Mkuu huku akishangiliwa.

Waziri Mkuu ambaye alienda kufanya usafi kwenye soko hilo, alilazimika kuzungumza na mamia ya wananchi waliofika
kushiriki zoezi hilo. Pia alikagua maeneo mbalimbali ya soko hilo hadi shimoni na kusema aneridhika na usafi uliofanyika bali amesisitiza usafi huo uendelezwe. “Kaulimbiu ya Mheshimiwa Rais Magufuli ya HAPA KAZI TU inatupa ari ya kufanya kazi. Fanyeni kazi. Watanzania mko huru

kufanya kazi yoyote lakini cha msingi fuateni taratibu na kanuni. Serikali hii tumamua kuwajali watu wa chini. Tutahakikisha wajasiriamali wadogo, akinamama lishe na wamachinga mnafanya kazi kwa amani na utulivu, ” alisema.
Rais Magufuli aliamua kuitangaza siku ya leo (Desemba 9, 2015) ambayo ni maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru iwe ni siku ya kufanya usafi nchi nzima ili kuepukana na magonjwa mbalimbali na hasa kipindupindu.