Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akikabidhiwa ili kuzindua mradi wa maboresho wa wa huduma za mahakama ya Tanzania kutoka kwa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe.Mohamed Chande Othman leo Kibaha Pwani.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akiweka jiwe la msingi la jengo la mahakama ya hakimu mkazi pwani na mahakama ya wilaya kibaha.Kushoto kwake ni Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe.Mohamed Chande Othman
Mufti Mkuu wa Tanzania Abubakar bin Zubeir Ally(katikati) akifuatilia Hotuba ya Waziri Mkuu wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati na mradi wa maboresho ya huduma za mahakama ya Tanzania uliofanyika leo Kibaha ,Pwani.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akizindua mpango mkakati wa miaka mitano(5) wa mahakama ya Tanzania ukilenga katika uboreshaji wa huduma za utoaji haki kwa mwananchi.Kushoto kwake ni Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe.Mohamed Chande Othman
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akiuliza swali kwa Mhadhiri kutoka chuo cha Ardhi , Idara ya Usanifu Dkt. Daniel A.Mbisso wakati alipokuwa akionyeshwa michoro ya mahakama leo Kibaha,Pwani.
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe.Mohamed Chande Othman akizungumza na mabalozi na viongozi waandamizi wa Serikali leo wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati na mradi wa maboresho ya huduma za mahakama ya Tanzania
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akikabidhi mradi wa maboresho ya huduma za mahakama ya Tanzania kwa mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi.Bella Bird leo KIbaha,Pwani.Benki ya Dunia imetoa shilingi milioni 141 kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa mahakama.