Waziri Mbarawa Ajisalili Mfumo wa Mahudhurio ya Kieletroniki

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  Profesa Makame Mbarawa akijisajili katika mfumo wa mahudhurio wa elektoniki (kulia), ni Afisa Utumishi Bi, Elizabeth Maduhu akimwelekeza.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akijisajili katika mfumo wa mahudhurio wa elektoniki (kulia), ni Afisa Utumishi Bi, Elizabeth Maduhu akimwelekeza.

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amezungumzia umuhimu wa taasisi zote za Serikali kuwa na mfumo wa mahudhurio kwa njia ya kielekroniki electronic attendance registration (EAR).

Akizungumza mara baada ya kujisajili katika ofisi za sekta ya mawasiliano Prof. Mbarawa amesema kwa kuanzia utaratibu huo utaendelezwa katika sekta Uchukuzi na Ujenzi na kisha utafungwa katika taasisi zote za Serikali ili kuhakikisha watumishi wa umma wanafika ofisini kwa wakati na kupunguza utoro.

“Hakikisheni watumishi wote wanatumia mfumo huu wa kielektroniki ili kudhibiti utoro na kuwezesha wafanyakazi kufanyakazi kwa muda unaokubalika kiserikali ”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Aidha Waziri Mbarawa amewataka wafanyakazi wa mapokezi kuacha kuwafungulia wafanyakazi watoro na wanaochelewa kazini kuingia ofisini ili kuwezesha mfumo kutambua watumishi watoro na hivyo kuchukuliwa hatua stahiki.

Amesisitiza kuwa mfumo huo utakapofungwa katika taasisi zote za umma utadhibiti watoro kwa kuwa unaweka kumbukumbu ya muda mtu anaokuwa kazini na hivyo kuwawezesha viongozi kupata taarifa sahihi za mahudhurio.