Waziri Kairuki Kutafuta Changamoto na Watumishi

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Anjella Kairuki (Mb), akitoa maelekezo kwa Watumishi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI mapema leo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Anjella Kairuki (Mb), akitoa maelekezo kwa Watumishi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais-UTUMISHI mapema leo.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Anjella Kairuki (Mb) amesema atakaa na Watumishi katika ofisi zao ili kubaini changamoto zinazowakabili na kuzitatua. Kairuki alisema hayo mapema leo wakati alipokutana na Wafanyakazi wa Idara ya Uendelezaji Sera-UTUMISHI katika kikao kazi.

“Watu wasiwe waoga katika kazi, mimi nimekuja kufanya kazi na kila kitu kina utaratibu wake” Mhe. Kairuki alisema na kusisitiza kuzingatia taratibu zilizowekwa ni jambo la msingi. Waziri Kairuki alisema kufanya kazi kwa ubunifu na kuwashirikisha Wafanyakazi wengine ili kutoa huduma bora na haraka kwa wananchi katika ulimwengu wa sasa ni muhimu.

Kairuki alielekeza katika mipango ni vizuri kuwa na maeneo maalum ambayo yatatoa huduma zaidi ya moja (Huduma Centre) ili kupunguza mzunguko usio lazima, na kuokoa muda kwa wananchi wanaofuata huduma hizo. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora, Anjella Kairuki (Mb) anakutana na kila Idara na Kitengo ndani ya ofisi yake ili kubaini changamoto na kuzitatua.