Waziri Dk Kigoda Azindua Bodi Chuo cha Elimu ya Biashara, CBE

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda (kulia) akimkabidhi mwongozo wa utendaji kazi Mwenyekiti wa Bodi iliyoteuliwa ya uongozi wa Chuo cha Elimu ya Biashara, Prof. Mathew Luhanga (kushoto) leo jijini Dar es Salaam. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda (kulia) akimkabidhi mwongozo wa utendaji kazi Mwenyekiti wa Bodi iliyoteuliwa ya uongozi wa Chuo cha Elimu ya Biashara, Prof. Mathew Luhanga (kushoto) leo jijini Dar es Salaam. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda (katikati) akizungumza jambo na viongozi na wajumbe wa Bodi mpya ya uongozi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) iliyoteuliwa alipokuwa akitembelea maeneo mbalimbali ya chuo hicho leo jijini Dar es salaam. Kutoka kushoto ni Mkuu wa chuo hicho Prof. Emanuel Mjema akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi Prof. Eleuther Mwageni na Prof. Mathew Luhanga ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi ya CBE (kulia).

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda (katikati) akizungumza jambo na viongozi na wajumbe wa Bodi mpya ya uongozi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) iliyoteuliwa alipokuwa akitembelea maeneo mbalimbali ya chuo hicho leo jijini Dar es salaam. Kutoka kushoto ni Mkuu wa chuo hicho Prof. Emanuel Mjema akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi Prof. Eleuther Mwageni na Prof. Mathew Luhanga ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi ya CBE (kulia).

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda akisalimiana na viongozi na wafanyakazi wa Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Dar es salaam alipowasili chuoni hapo kuzindua Bodi mpya ya uongozi ya Chuo hicho leo. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda akisalimiana na viongozi na wafanyakazi wa Chuo cha Elimu ya Biashara kampasi ya Dar es salaam alipowasili chuoni hapo kuzindua Bodi mpya ya uongozi ya Chuo hicho leo. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Na Aron Msigwa – MAELEZO, Dar es Salaam

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda amezindua rasmi Bodi ya Uongozi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na kuitaka bodi hiyo kufanya kazi zake kwa kuzingatia sheria na kushirikiana na menejimenti ya chuo hicho kuweka mikakati na mipango ya maendeleo itakayokiwezesha chuo hicho kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.

Akizungumza na viongozi na wajumbe wa bodi hiyo leo jijini Dar es salaam, Dk. Kigoda amesema serikali inayo imani kubwa na Mwenyekiti na wajumbe wa Bodi hiyo walioteuliwa na kwamba watatimiza majukumu yao kikamilifu na kukiwezesha chuo hicho kufikia malengo na matarajio ya Watanzania ya kuendelea kuzalisha wataalam bora wa fani za biashara.

“Ninaamini kuwa Bodi niliyoizindua leo itasimamia shughuli za chuo hiki kwa kufuata misingi ya uadilifu, utawala bora na kuongeza chachu ya kuleta huduma bora kwa wananchuo na umma,” Amesisitiza Dk. Kigoda.

Alisema viongozi na wajumbe wa Bodi walioteuliwa wanalojukumu la kusimamia ustawi wa chuo hicho wakiwa chombo cha juu cha utoaji wa maamuzi na usimamizi wa masuala mbalimbali ya chuo hicho ikiwemo uidhinishaji wa matumizi ya chuo yanayoendana na mapato ya chuo, uteuzi wa Mkuu wa Chuo na watumishi wengine na uidhinishaji wa viwango vya ada.

Akizungumzia mabadiliko ya chuo hicho toka kuanzishwa kwake mwaka 1965 Dk. Kigoda amesema yamehusisha mabadiliko makubwa ya mitaala ya kufundishia ili kuwafanya wanafunzi na wahitimu waweze kupanua ufahamu wao kwa kuwa na uwezo wa kukabiliana na ushindani wa soko la ajira kwa kuongeza fursa za ajira katika sekta ya umma na binafsi pamoja kuwajengea uwezo wahitimu waweze kujiajiri wenyewe.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Prof. Emanuel Mjema akizungumza wakati wa kuwakaribisha wajumbe walioteuliwa chuo hapo amesema kuwa wao kama viongozi wa chuo hicho wataendelea kusimamia msingi wa kuanzishwa kwa chuo wa kuendelea kuzalisha wataalam bora katika nyanja za biashara na sekta ya uendeshaji viwanda nchini.

Amesema kuwa wao kama menejimenti ya chuo hicho watashirikiana na uongozi na wajumbe wa bodi iliyoteuliwa kusimamia rasilimali na miundombinu ya chuo hicho ili kiendelee kutoa huduma bora kwa wanafunzi na wananchi wengi Zaidi kwa wakati.

Naye Makamu mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi ya Chuo hicho Prof. Eleuther Mwageni akizungumza kwa niaba ya uongozi na wajumbe wa bodi iliyoteuliwa amesema kuwa Bodi iliyoteuliwa  itatekeleza majukumu yote yaliyoanishwa kwa mujibu wa sheria.