WAZIRI wa Elimu na Mafunzo, Dk. Shukuru Kawambwa, jana Julai 7, 2014, alitembelea maenesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (TANTRADE), yajulikanayo kama maonesho ya Saba Saba, na kutembelea Banda la Shule ya Sekondari Imperial, Dk. Kawambwa ametoa pongezi kwa uongozi na waalimu wa Shule ya Sekondari Imperial, kwa Jinsi ilivyojipanga kuhakikisha inatoa Elimu Bora Nchini, inayokidhi viwango vya Kimataifa, kwa gharama nafuu.
Shule ya Sekondari Imperial, iko Msolwa-Chalinze. Shule imejengwa katika eneo lenye ukubwa wa hekari 27, lililopo Plot No. 1, Block C, Msolwa-Chalinze. Shule inafundisha na kutoa mtaala “Curriculum” wa hapa hapa nyumbani, yaani NECTA na Mtaala wa IGCSE “Cambridge Curriculum”
Wanaopenda kujiunga au kuandikisha watoto wao kwa mwaka wa Taaluma unaanza Tarehe 5 Januari,-2015, fomu ni chache na zinapatikana kwa anuani zifuatazo:
www.imperial.ac.tz
principal@imperial.ac.tz
0758 50 51 52
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi , Dr. Shukuru Kawambwa akiingia katika banda la shule ya sekondari Imperial.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dr. Shukuru Kawambwa akisaini kitabu cha wageni wakati apotembelea banda la shule ya sekondari ya Imperial Kushoto ni Mama Iryna Kanyoko Mkuu wa shule hiyo.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dr. Shukuru Kawambwa akifurahia jambo wakati alipokuwa akizungumza na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Imperial Mama Iryna Kanyoko alipotembelea katika banda lao kwenye viwanja vya Sabasaba
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Imperial Mama Iryna Kanyoko akimtambulisha Waziri wa Elimu na Mafunzo na Ufundi , Dr. Shukuru Kawambwa baadhi ya walimu wa shule hiyo.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dr. Shukuru Kawambwa akizungumza na baadhi ya wakuu wa idara za shule ya sekondari ya Imperial iliyoko Msolwa Chalinze mkoani Pwani.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi , Dr. Shukuru Kawambwa akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa shule ya sekondari ya Imperial Mama Iryna Kanyoko, kutoka kulia ni Mwalimu wa taaluma Bw. Juma na Dr. Mwingira Daktari wa shule ya sekondari Imperial