
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na Gavana wa Jimbo la Maryland la nchini Marekani, Mhe. Martin O’Malley walipokutana jijini Washington D.C kwa mazungumzo kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Jimbo hilo na Tanzania katika masuala ya uchumi, jamii na siasa. Mhe. Membe alipata fursa ya kukutana na Gavana huyo alipokuwa mjini humo kwa ajili ya kumwakilisha Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye upokeaji Tuzo ya Kiongozi mwenye Mchango Mkubwa zaidi katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa Mwaka 2013.
Mhe. Gavana O’Malley akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula |
Mhe. Waziri Membe akitoa salamu maalum kwa wajumbe kabla ya mkutano kuanza. Pembeni ni Mhe. Gavana O’Malley. |
Mhe. Membe akizungumza huku Gavana O’Malley akimsikiliza. |
Mhe. Membe akiendelea na mazungumzo huku Mhe. Gavana O’Malley na wajumbe wengine wakimsikiliza. |
Mhe. Gavana O’Malley akizungumza. |
Balozi Mulamula akiwa na wajumbe wengine wakimsikiliza Gavana O’Malley (hayupo pichani) |
Wajumbe wengine wakati wa mkutano kati ya Mhe. Membe na Gavana O’Malley (hawapo pichani). Kushoto ni Bw. Thobias Makoba, Katibu wa Waziri Membe na Bi. Redemptor Tibaigana, Afisa Mambo ya Nje. |
Wajumbe wengine |
Mhe. Membe akimweleza jambo Mhe. Gavana O’Malley mara baada ya mazungumzo yao. |
Mhe. Gavana O’Malley katika picha ya pamoja na Bal. Mulamula |
Mhe. Gavana O’Malley katika picha ya pamoja na Bi. Kasiga. |
Mhe. Membe na Mhe. Gavana O’Malley katika picha ya pamoja na wajumbe wengine. |