Wazee CCM waunga mkono Rostam kujivua gamba

BARAZA la Wazee wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Dar es Salaam limesema uamuzi uliofanywa na aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Igunga Rostam Azizi ni uamuzi wa kawaida na si kwanza kufanya hivyo.

Limesisitiza kuwa hata aliyekuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Makamu wa Rais wa Kwanza kwa Serikali ya Jamuhuri ya Muungamo wa Tanzania Aboud Jumbe Mwinyi alishawahi kufanya uamuzi kama huo na bado chama kilibaki imara na kusonga mbele.

Wakizinmguza Dar es Salaam jana wazee hao walisema kuwa alichokifa nya Rostam kuamua kujivua gamba ni mambo ambayo yanaweza kuzungumzwa na kufafanuliwa vizuri na viongozi wa chama hicho lakini kwa nafasi yao wanaona in uamuzi wa kawaida.

Baraza Hilo lilikutana kwa ajili ya kujadli ajenda mbili ikiwemo ya kumteua Idd Simba kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa wa CCM Dar es Salaam baada ya kuwa wazi kutokana na kufariki kwa mzee Athuman Mwinyimvua Mei mwaka huu.

Akizungumwa kwa niaba ya baraza za wazee hao, Kaimu Mwenyekiti wazee hao Hemed Mkali alisema kuwa Rostam ameamua kupumzika hivyo kama ilivyokuwa kawaida ya chama hicho wengine watachukua kiti na kuendeleza pale alipoishia.

Alisema hakuna sababu ya wao kuanza kuzungumzia uamuzi wa Rostam kuhusu kuacha kuwa mbunge way Jimbo la Igunga lakini bado akafafanua kuwa mzee Jumbe alipoamua kuchukua uamuzi wa kupumzika kwa sasa yupo Kigamboni Dar es Salaam ambapo ameendelea kuwa mwanachama way CCM.

“Tunakumbuka , mzee Jumbe ameshika nafasi kubwa katika nchi hii za uongozi kuliko Rostam lakini bado aliona kuna haja ya kuacha majukumu yake ya uongozi na kuacha wengine waendelee kukimbiza kijiti .Hivyo uamuzi way Rostam in wa kawaida na tunaamini alichokifanya ameamua kupumzika kushikilia nyadhifa alizokuwa nazo ndani ya chama,”alisema Mkali.

Hata hivyo Mkali alishindwa kuzungumzia zaidi mwenendo wa CCM kwa sasa ambapo hali ya kisiasa inaonekana kuwa tete ndani ya chama chao lakini akatumia nafasi hiyo kufafanua kuwa kazi yao kubwa in kutoa ushauri ili chama kiweze kusonga mbele.

Wiki hii Rostam aliamua kujivua gamba ambapo alisema amefikia uamuzi huo kutokana na kuchoshwa na siasa za Tanzania ambazo zimekuwa siasa uchwara za kupakana matope jambo ambalo linamfanya kuwa katika wakati mgumu katika shughuli zake za kibiashara.

Mkali akizungumzia uamuzi way kumteua Simba kushika nafasi hiyo ya kuwaongoza wa wazee wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam kuwa ilikuwa wazi ndio maana wameona ipo haja ya kuzibwa nafasi hiyo ili waweze kuendelea na mambo yao ya kukishauri chama kazi ambayo wamekuwa wakiifanya kabla na baada ya Uhuru wa Tanzania.