Mkurugenzi mtendaji wa shule ya Southern Highlands Mafinga Bi Mary Mungai kushoto akiwa na wageni mbalimbali |
Wanafunzi wa shule ya Southern Highlands Mafinda wakipiga vyombo vya muziki walipokuwa wakiimba wimbo wa Taifa siku ya mahafali ya chekechea na siku ya wazazi shuleni hapo |
Mwalimu Bi Sarah akijitambulisha mbele ya wazazi |
Wageni mbalimbali wakiwa katika hafla ya siku ya wazazi |
WAZAZI wa wanafunzi wanaosoma shule ya Kimataifa ya Southern Highlands Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wamechangia kiasi cha zaidi ya Tsh milioni 5 kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za uongozi wa shule hiyo kuanzisha shule ya sekondari inayojulikana kwa jina la Mufindi Highlands School.
Michango hiyo ambayo ni fedha taslimu na ahadi ilitolewa jana wakati wa mahafali ya chekechea na siku ya wazazi shuleni hapo kufuatia wazazi hao kuvutiwa na taarifa ya mkurugenzi wa shule hiyo kuhusu uanzishwaji wa shule mpya ya sekondari.
Mmoja kati ya wazazi hao Blankson Ponela ambae alijitolea ahadi ya kuachangia kiasi cha Tsh milioni 1.5 alisema kuwa amevutiwa zaidi na jitihada za uongozi wa shule hiyo kwa kuanzisha shule ya sekondari yake.
Kwani alisema kuwa awali wanafunzi wanaofaulu katika shule hiyo wamekuwa wakipata wakati mgumu kuzoea mazingira ya shule za sekondari ambazo wanafunzi wake wametoka katika shule za msingi za serikali ambao uwezo wao huwa na chini ya ule wa wanafunzi waliotoka katika shule hiyo ya Southern Hihglands ambayo wanafunzi hujifunza lugha mbali mbali ikiwemo ya Kiingereza na kifaransa na Kiswahili.
“Tunapenda kuupongeza uongozi wa shule hii kwa kuja na wazo la kuwa na shule ya sekondari yake ambayo itawachukua wanafunzi wanaofaulu katika shule hii ya msingi …binafsi na familia yangu kwa ajili ya kuunga mkono hili ninaahidi kuunga mkono kwa kuchangia kiasi cha
Tsh milioni 1.5 ili kufanikisha ujenzi huo,” Huku Bw Peter Ole Mamasita alisema kuwa kwa mkoa wa Iringa shule hiyo ya Southern ndio imeendelea kuwa shule yenye rekodi nzuri ya ufaulu wa wanafunzi ukilinganisha na shule nyingine za binafsi na serikali.
Hivyo alisema kuanzishwa kwa shule hiyo ni imani kubwa kwa wazazi katika wilaya ya Mufindi na nje ya wilaya hiyo kuendelea kunufaika na matunda ya shule hiyo hasa kwa kuendelea kuwafanya watoto wao kupata elimu ya chekechea ,msingi hadi sekondari wakiwa katika eneo moja badala ya kuanza kutafuta shule nyingine nje ya wilaya hiyo.
Mkuu wa shule hiyo Jonson Nyabuto alisema kuwa shule hiyo kwa huu 2014 ilikuwa na wanafunzi 48 na wote walifaulu kujiuga na sekondari na kuifanya shule hiyo katika matokeo ya mtihani huo kitaifa kwa wilaya kushika nafasi ya kwanza kati ya shule 167 kimkoa nafasi ya nane kati ya shule 458 na kitaifa kuwa shule ya 353 kati ya shule zaidi ya 15,867 hivyo kwa matokeo hayo shule hiyo imeweza kupanda kwa wastani wa pointi tano zaidi ya mwaka jana.
Alisema kwa mwaka jana shule hiyo ilifaulisha pia wanafunzi wote 47 na kushika nafasi ya pili kiwilaya nafasi ya 9 kimkoa na kitaifa kuwa shule ya 288.
Mkurugezi mtendaji wa shule hiyo Mary Mungai alisema kuwa ujenzi wa shule hiyo kwa awamu ya kwanza unategemea kugharimu kiasi cha Tsh milioni 50 kwa kujenga mabweni mawili kwa ajili ya wavulana na
wasichana pamoja na madarasa manne na nyumba moja ya mwalimu . Aliwaomba wadau mbali mbali wa ndani ya nchi na nje ya nchi kusaidia ujenzi huo wa shule ya sekondari kwa kuchangia michango yao kwa M-Pesa 0754651966 ama 0752840884 kwani alisema upatikanaji wa fedha hizi ni mgumu zaidi iwapo ataufanya peke yake ila kama wadau mbali mbali wataunganisha nguvu zao uwezekano wa kumaliza ujenzi huo kwa wakati upo. Hata hivyo alisema awamu ya pili itakuwa ujenzi wa maabara ya kiasasa, kuongeza nyumba vya madarasa, nyumba za walimu na kuwa shule hiyo inatarajiwa kujengwa kwa awamu tatu hadi kukamilika kwake na jumla ya Tsh bilioni 1 ndizo zinahitajika ili kukamilisha ujenzi
wa shule hiyo ya sekondari japo alisema mchakato wa kuanza kupokea wanafunzi kwa ajili ya kuanza kidato cha kwanza utaanza mapema mwaka huu na mwakani shule hiyo ya Southern Highlands Mafinda itakuwa pia na wanafunzi wa kidato cha kwanza kupitia shule yake ya sekondari ya Mufindi Highlands School.
Mkurugenzi huyo alisema kwa wazazi wanaotaka watoto wao kujiunga na shule hiyo nafasi za masomo kuanzia chekechea , darasa la kwanza hadi la tatu wanaotokea kiswahili medium schools na la tano pia wakati, Darasa la 4 na 6 wanaotoka English medium.
Huku wale wa la nne na sita wale wanaotoka English medium schools wanaweza kujiunga na shule hiyo kwa kujaza fomu za kujiunga
zinazopatikana shuleni Mafinga na kutakuwa na interviews tarehe 13 / 12/2014 maeneo yafuatayo. Shuleni Southern Highlands Mafinga, Oyster Bay Primary school, Dar es salaam, chuo cha Nursing Ilembula na Misufini primary school, Songea ama kuwasiliana na uongozi wa shule kwa simu hii 0756749151 au 0754651966 Pia alisema sekondari form one wanazo nafasi na jina la sekondari; Mufindi Highlands School
Alisema kuwa shule hiyo ni moja kati ya shule bora katika wilaya ya Mufindi na mkoa wa Iringa pamoja na Taifa na kwa kuwa toka ianzishwe kwake haijapata kufelisha hata mwanafunzi mmoja zaidi ya kufaulisha wanafunzi wote darasa la saba . |