
Ujumbe wa Tanzania (Kulia) ukiongozwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda wakiwa katika kikao maalum na ujumbe wa Bunge la Japan (kushoto) uliongozwa na Mwenyeji wake Spika wa Japan, Takahiro Yokomichi. Makinda yupo Japan kwa mwaliko maalum na Bunge la Japan kwa lengo la kujadili na kuimarisha ushirikiano baina ya Mabunge haya mawili.