Wauwawa Wakitoa Chanjo ya Polio Nigeria

Wahudumu wakitoa chanjo ya polio

RIPOTI kutoka nchini Nigeria zinasema kuwa watu 12 wakiwemo wafanyakazi waliokuwa wanatoa chanjo ya Polio kwa watoto, wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana. Maofisa wa afya nchini Nigeria wamewaeleza wanahabari kuwa wafanyakazi wanane waliokuwa wanatoa chanjo waliuawa mjini Kano na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Taarifa zaidi kutoka kwa watu walioshuhudia mauaji hayo zinasema kuwa, watu wengine 8 waliuawa katika kituo cha afya maeneo ya Hotoro, karibu na Mji wa Kano. Miongoni mwa waliouawa ni wanawake waliokuwa wanawasubiri watoto wao, waliokuwa wanachanjwa. Baadhi ya viongozi wa kiisilamu, Kaskazini mwa Nigeria wamekuwa wakipinga chanjo ya Polio, wakisema inasababisha watu kukosa uwezo wa kuzaa.
-BBC