SERIKALI nchini Kenya imewafukuza kazi wauguzi 25,000 waliogoma kwa kushindwa kurudi kazini.
Msemaji wa Serikali hiyo, Alfred Mutua amewataka watu wote wenye taaluma ya afya na ambao hawakuwa na ajira au waliostaafu kufika hosiptali za umma kwa ajili ya kuajiriwa siku ya Ijumaa kuziba nafasi ya wauguzi hao.
Taarifa kutoka Kenya zinasema wafanyakazi wa umma ambo wengi ni manesi waligoma tangu wiki iliyopita wakitaka kupandishiwa mishahara, marupurupu na kuboreshewa mazingira ya kazi wametimuliwa. Hata hivyo vyama vya wafanyakazi wamepuuzia hatua hiyo wakisema ni mbinu ya kuwataka wajadiliane.
“Huu ni mchezo wa paka na panya, huwezi kuwafuta kazi wafanyakazi wote. Ni mbinu yao tu ya kutufanya haraka turudi kazini lakini mgomo wetu unaendelea mpaka madai yetu yakamilishwe,” alisema, Alex Orina, Msemaji wa Taasisi ya wanataaluma wa afya nchini Kenya.
Alisema kwa wastani mfanyakazi wa sekta ya afya anapata kiasi cha sh. 25,000 za Kenya ($300, £190) kwa mwezi kwenye mshahara wake na posho. Lakini, Mutua alisema wafanyakazi wa afya ‘hawaufuata maadili’ kwa kutorejea kwenye majukumuyao.
Alisema majinayaoyameondolewa katika orodha ya wafanyakazi wanaolipwa mshahara na si ‘waajiriwa wa serikali tena’. Dk. Victor Ng’ani, mwenyekiti wa Wafanyakazi wa Afya, wafamasia na wataalam wa meno alisema ulikuwa ni uamuzi wa ‘kizembe.’
Aliiambia BBC kuwa itakuwa vigumu kuwapata wafanyakazi mbadala kuziba nafasi ya miaka mingi ya watu wenye uzoefu na ujuzi wa kazi maalum.
-BBC