Watumiaji Kiswahili Nchini Japan Wazidi Kuongezeka

Watumiaji Kiswahili Nchini Japan Wazidi Kuongezeka

Mshindi wa droo ya kwanza ya promosheni ya WINDA NA USHINDE inayoendeshwa na kampuni ya Bia ya Serengeti(SBL) Honest Minja akiongea na wadau waliohudhuria hafla hiyo

Na Anna Nkinda – Yokohama

WATUMIAJI wa lugha ya Kiswahili wamezidi kuongezeka nchini Japani hadi kufikia hatua ya kuwa na mshindano kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Soka kilichopo nchini humo. Hayo yamesemwa leo na Prof. wa chuo hicho Midori Uno wakati akiongea na Mke wa Rais mama Salma Kikwete alipokutana naye katika hoteli ya Intercontinental mjini Yokohama.

Prof. Uno ambaye ni Mwalimu wa kiswahili katika chuo hicho alisema kuwa hivi Sasa wananchi wengi  wa Japani wanakiu ya kujifunza na kuzungumza lugha ya Kiswahili kwani ni rahisi kueleweka.

“Katika jitihada zangu za kuwafanya wajapani wengi wajue lugha ya Kiswahili nimetengeneza kamusi ya maneno ya kijapani kuwa ya Kiswahili ambayo watu wengi wanaitumia kwa sasa kwani wengi wajapani wengi wanapenda kujifunza lugha hii”, alisema Prof. Uno.

Mashindano hayo ya lugha ya Kiswahili ambayo hufanyika mwezi wa kumi na moja kila mwaka huwa ni ya kuandika na kusoma hotuba ambapo mshindi wa kwanza anapewa cheti, tuzo ya muanzilishi wa chuo hicho, vikombe na zawadi mbalimbali. Kwa upande wake Mke wa Rais mama Kikwete alimpongeza profesa huyo kwa jitihada zake za kukuza lugha ya Kiswahili nchini humo na kumuomba aendelee zaidi kufanya hivyo.

Alisema kuwa watanzania wanavitu vyao vya kujivunia kama Taifa, moja ya vitu hivyo ni lugha ya Kiswahili ambayo imewaunganisha  watanzania wote na kuwa kitu kimoja ndani na n je ya nchi.
Mama Kikwete alisema, “Ili kumfikia mtu mmoja au watu wengi zaidi ni lazima kuwe na lugha ya mawasiliano hivyo basi nasi tunatumia lugha hii ambayo iliwaunganisha watanzania wote wakaweza kupigania uhuru wa n chi yao kipindi cha mkoloni”.

Alisema kuwa lugha ya Kiswahili inaongelewa maeneo mengi ya Afrika ya mashariki na ndani ya bara la Afrika na hivi sasa viongozi wa Umoja wa Nchi za Afrika (AU) waliikubali lugha hiyo kuwa lugha ya mawasiliano.

Profesa Uno alikuja nchini kabla ya kupata uhuru kwa ajili ya kufanya kazi za kujitolea na aliporudi nchini kwake aliamua kuwafundisha wajapani lugha ya Kiswahili pia nchini humo redio Japani (NHK) inatangaza matangazo yake kwa lugha ya Kiswahili ambayo ilianzishwa mwaka 1964.