WATU takriban 15 wameuwawa na wengine 79 kujeruhiwa kufuatia mlipuko uliotokea katika mji mkuu wa Myanmar, Yangon. Maafisa wanasema mlipuko huo ulisababisha moto kwenye ghala linalomilikiwa na serikali, ambao ulienea kwa kasi katika makazi ya watu na majengo mengine yaliyokuwa karibu, mengi yao yakiwa ya mbao. Wazima moto wanaendelea na juhudi za kuuzima moto huo na kuzitafuta maiti. Duru za hospitali zinasema afisa mmoja wa zima moto ameuwawa wakati walipojaribu kuuzima moto huo. Haikubainika mara moja kilichousababisha mlipuko huo.
-DW