Watu 50 Wafukiwa na Kifusi, 20 Wauwawa kwa Bomu Somalia

Watu 50 Wafukiwa na Kifusi, 20 Wauwawa kwa Bomu

WATU wawili wamefariki na wengine takriban 50 kukwama kwenye kifusi cha jengo baada ya paa la jumba la maduka lililokuwa likijengwa kuporomoka nchini Afrika Kusini. Inaarifiwa watu 29 wameweza kuokolewa.

Madaktari kutoka kampuni binafsi ya Netcare 911 walifika kutoa huduma ya kwanza katika eneo hilo la Tongaat Kaskazini mwa Mji wa Durban.

“Shughuli hii itachukua mda mrefu. Itatuchukua muda kuwafikia wale waliokwama,” alisema msemaji wa kampuni hiyo. Hata hivyo ni mapema mno kujua sababu ya kuporomoka kwa jengo hilo. Inaarifiwa watu wengine 26 wamepelekwa hospitalini wakiwa na majereha mabaya.

Wakati huo huo; watu ishirini wameuawa katika shambulio la kujitoa mhanga kwenye kituo cha polisi nchini Somalia. Shambulio hilo limetokea katika Mji wa Beledweyne karibu na mpaka na Ethiopia.

Mashuhuda wameiambia BBC kuwa gari lilipiga lango kuu la kuingia kwenye jengo la polisi na kulipuka kabla ya watu wenye silaha kushuka na kushambulia jengo hilo kwa risasi. Taarifa zinasema wengi waliofariki katika shambulio hilo ni maafisa wa polisi.

Taarifa zinazohusianaSomalia, alshababMwandishi wa habari wa BBC nchini Somalia Mohammed Moalimu amesema kituo hicho cha polisi kipo karibu na ngome ya majeshi ya Umoja wa mataifa yaliyopo nchini Somalia AMISOM.

Wapiganaji wa kiislamu wa Al Shabaab wamekiri kuhusika na shambulio hilo. Mwezi uliopita wapiganaji hao wa Al Shabaab pia walikiri kuhusika na shambulio jingine ambapo watu 16 waliuawa katika hoteli moja maarufu mjini Mogadishu. Maofisa wa polisi nchini Somalia wamesema mlipuko huo ulikuwa ni mkubwa na umesababisha majeruhi kadhaa.

“Mlipuko ulikuwa ni mkubwa na pia wapo majeruhi kadhaa, hata hivyo hali imedhibitiwa,” amesema Kanali Abdulkadir Ali, kamanda wa polisi wa mji huo wakati akizungumza.

Kamanda wa kundi la Al Shabaab Mohamed Abu Suleiman ameliambia shirika la AFP kuwa makomandoo wa Al Shabaab ndio waliofanya shambulio hilo.

Naye Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amesema shambulilo hilo ni la kujimaliza na linaonyesha kutojali maisha.

“Kipau mbele changu cha kwanza ni kutuma salamu za rambi rambi kwa waathirika na familia zilizoguswa na tukio hilo la kipumbavu”, alisema katika taarifa yake

“Nimesema ni shambulio la kipumbavu kwa sababu maadui zetu wanapaswa kuelewa kwamba mashambulizi hayatawasaidia kuendeleza harakati zao zaidi sana yanawapotosha”

Mwezi Septemba, kundi la Al Shabaab lilisema kuwa lilifanya shambulizi la kigaindi katika kituo cha biashara cha Westgate nchini Kenya ambapo watu wapatao 67 waliuawa.

-BBC